Monday, 7 August 2017
WIZARA YA AFYA, MEANDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.
 


TAARIFA KWA UMMA
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anatarajia kuhakiki Mashirika yote Yasiyo ya Kiserikali kuanzia tarehe 21 hadi 31 Agosti, 2017. Lengo kuu la zoezi hili ni Kuhuisha orodha ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini, Kuboresha Kanzi Data ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kupima utekelezaji wa majukumu ya Mashirika haya. Zoezi hili litafanyika katika Kanda tano (5). Kanda ya Mashariki itahudumia mikoa ya DAR ES SALAAM, LINDI, MTWARA, PWANI na MOROGORO na Kituo kitakuwa Idara ya Uratibu wa NGOs DAR ES SALAAM;  Kanda ya Kati itahudumia mikoa ya DODOMA, SINGIDA, TABORA na KIGOMA na Kituo kitakuwa DODOMA, Makao Makuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliyopo Chuo Kikuu cha Dodoma,  Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii, Jengo Na. 11, Dodoma; Kanda ya Kaskazini itahudumia mikoa ya KILIMANJARO, TANGA, ARUSHA na MANYARA na Kituo kitakuwa katika Ofisi ya Katibu Tawala (M) KILIMANJARO; Kanda ya Ziwa itahudumia mikoa ya MWANZA, KAGERA, MARA, GEITA, SIMIYU na SHINYANGA na Kituo kitakuwa katika Ofisi ya Katibu Tawala (M) MWANZA na Kanda ya Nyanda za Juu - Kusini itahudumia mikoa ya MBEYA, RUVUMA, KATAVI, RUKWA, SONGWE, NJOMBE na IRINGA na Kituo kitakuwa katika Ofisi ya Katibu Tawala (M), MBEYA.
Wakati wa uhakiki kila shirika linapaswa kuwasilisha Cheti Halisi cha Usajili, Nakala ya Cheti cha Usajili, kujaza fomu ya uhakiki NGO-Fomu/UHK/2017 inayopatikana katika Tovuti (www.tnnc.go.tz), Stakabadhi za Malipo ya Ada ya mwaka toka kuanzishwa kwa shirika, Barua kutoka kwa Afisa Maendeleo ya Jamii (Mkoa/Wilaya/Halmashauri/Manispaa) ikithibitisha uwepo wa Ofisi ya Shirika na nakala ya katiba iliyothibitishwa na Msajili wa NGOs. Aidha, Mashirika yote yatakayoshindwa kuhakikiwa katika vituo vya Kanda tajwa hapo juu, yatafutiwa Usajili na kuondolewa kwenye Regista ya Msajili wa NGOs. Ili kutoa fursa ya kuhuisha Kanzi Data na Benki ya Takwimu, Usajili wa NGOs utasitishwa kuanzia tarehe 21 Agosti hadi 30 Novemba, 2017.

M.S. Katemba
MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

Friday, 9 June 2017WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO                                     TANGAZO


WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO INAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KWAMBA
IMEANZA KUPOKEA MAOMBI YA WANAOTAKA KUJIUNGA NA MASOMO KATIKA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII
(CDTIs) NA MAENDELEO YA JAMII UFUNDI (CDTTIs).
VYUO VINAVYOTOA KOZI YA MAENDELEO YA JAMII NI BUHARE, MLALE, MONDULI, RUAHA, RUNGEMBA NA UYOLE.
VYUO VINAVYOTOA KOZI YA MAENDELEOYA JAMII UFUNDI (CIVIL ENGINEERING) NI MABUGHAI NA MISUNGWI.
SIFA ZA KUJIUNGA

A. VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII
1. NGAZI YA CHETI CHA AWALI –NTA LEVEL 4:
Muombaji awe amehitimu kidato cha nne na ana ufaulu ufaulu wa angalau wa alama D katika masomo 4
Au
 Awe na Cheti cha VETA (NVA Level 3)

2. NGAZI YA CHETI (ASTASHAHADA) –NTA LEVEL 5:
Muombaji awe amehitimu NTA LEVEL 4 kwa ufaulu wa daraja la PASS katika Fani ya Maendeleo ya Jamii au
inayoshabihiana na Maendeleo ya Jamii
Au
Awe amehitimu kidato cha sita kwa ufaulu wa angalau alama ya PRINCIPAL 1

3. NGAZI YA DIPLOMA (STASHAHADA)- NTALEVEL6:
Muombaji awe amehitimu Astashahada (NTA level 5 ) kwa ufaulu wa angalau daraja la PASS katika fani ya
Maendeleo ya Jamii au inayoshabihiana na Maendeleo ya Jamii

B. VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII NA UFUNDI (CIVIL ENGINEERING)
1. NGAZI YA CHETI CHA AWALI –NTA LEVEL 4:
Muombaji awe amehitimu kidato cha nne na anaufaulu ufaulu walau wa alama D katika masomo 4 mawili kati ya
hayo yatokane na FIZIKIA au KEMIA au HISABATI au KINGEREZA.
Au
Awe amemaliza kidato cha nne kwa ufaulu wa alama D katika masomo 4 na Cheti cha VETA (NVA Level 3)
2. NGAZI YA CHETI (ASTASHAHADA) –NTA LEVEL 5:

Muombaji awe amehitimu NTA LEVEL 4 kwa ufaulu wa daraja la PASS katika Fani ya Maendeleo ya Jamii na
Ufundi (Civil Engineering) au inayaoshabihiana nayo.
AU
Awe amehitimu kidato cha sita kwa ufaulu wa angalau alama za PRINCIPAL 1 na SUBSIDIARY 1 katika
michepuo ya PCM au PGM au PCB au EGM.

3. NGAZI YA DIPLOMA (STASHAHADA)- NTALEVEL6:
Muombaji awe amehitimu Astashahada (NTA level 5 ) kwa ufaulu wa angalau daraja la PASS katika fani
Maendeleo ya Jamii na Ufundi (Civil Engineering) au inayaoshabihiana nayo.
 Kwa maelezo zaidi wasiliana na wakuu wa vyuo kupitia namba zifuatazo
 Buhare-0752 760981/0766 844264
 Mlale- 0712 719532
 Uyole- 0754 576455 /0755 047572
 Ruaha- 0658 204835
 Rungemba-0763 375625/ 0625 724507
 Monduli- 0754 466803
 Missungwi- 0743 520523/0766 004212
 Mabughai- 0784 647063/ 0755 322454

 NB: Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20/08/2017

Tuesday, 6 June 2017

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
(IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KAULIMBIU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA JUNI 16, 2017

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na asasi za kiraia itaungana na mataifa mengine barani Afrika kusherehekea sikuu ya mtoto wa Afrika kwa Mwaka 2017 Kitaifa mkoani Dodoma tarehe 16 Juni mwaka huu.

Wizara inatoa taarifa kwa vyombo vya habari pamoja na wadau wengine kuwa, Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka huu 2017 ni Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa sawa kwa Watoto”.

Wizara inatoa wito kwa  vyombo vya habari waandishi wa habari kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika kuelimisha jamii kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu ambayo inahimiza uzingatiaji wa jukumu la ulinzi na usalama wa Mtoto na utoaji wa haki sawa kwa watoto wote ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo mwaka 2030.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)
06/6/2017


Friday, 2 June 2017

Baadhi ya  Wajumbe walioshiriki mafunzo ya Mkakati wa Kitaifa Kukomesha ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto leo mjini Morogoro wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo leo jijini Morogoro.
Wajumbe walioshiriki mafunzo ya Mkakati wa Kitaifa Kukomesha ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto leo mjini Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi kutoka Wizara ya Aya(Idara kuu Maendeleo ya Jamii aliyesimamana Bwana .Charlse Mafwimbo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera akisoma hotub  kwa wajumbe wa Mkutano wa walioshiriki mafunzo ya Mkakati wa Kitaifa Kukomesha ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto leo mjini Morogoro.        
Baadhi ya  Wajumbe walioshiriki mafunzo ya Mkakati wa Kitaifa Kukomesha ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto leo mjini Morogoro wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo leo jijini Morogoro
Wanawake na watoto nchini Tanzania wamekuwa wakifanyiwa  ukatili kwa kisingizio cha mila na desturi huku jamii ikishuhudia au kusikia wanawake na watoto wakipigwa na wakati mwingine kubakwa na hata kuuwawa na watu wa karibu ikiwemo waume au wapenzi wao.
Utafiti wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2016 unaweka bayana kuwa  Nchi za Afrika zilizochini ya Jangwa la Sahara zinaingia hasara ya dolla billion 95 sawa na shilingi trilioni 212 kila mwaka kutokana na kukosa usawa wa kijinsia na  kuendelea kuwepo kwa  vitendo vya ukatili wa kijinsia. Hali  hii ni ushahidi tosha kuwa vitendo vya ukatili vina madhara makubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.
Amesema hayo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo  ya   Jinsia  Bw.Julius Mbilinyi wakati akisoma  hotuba kwa niaba ya  Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  - Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga wakati wa ufunguzi wa Mafunzo Kuhusu Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto, kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii  wa Asasi za Kiraia leo Mjini Morogoro.
Bw. Mbilinyi ameongeza kuwa tafiti  mbalimbali ikiwemo Taarifa kuhusu Idadi ya Watu na Afya wa mwaka 2015-2016  inaonesha kuwa idadi  ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa nchini bado ipo juu ambapoTaarifa hii inaonesha kuwa “wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.
Aidha Ukatili wa kimwili unaongezeka kadri umri unavyoongezeka na Asilimia 22 ya wanawake wenye umri wa miaka 15-19 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili, ukilinganisha na asilimia 48 ya wanawake wenye umri wa miaka 40-49”. 
Aliongeza kuwa madhara ya vitendo vya ubaguzi,  unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto vimeathiri na vinaendelea kuwaathiri kiafya, kisaikolojia na kijamii wahanga wa vitendo hivi. Hali hiyo pia inaathiri ushiriki wao katika shughuli za kijamii, kiuchumi, kisiasa na maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.  
Aidha katika kukabiliana na changamoto ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Wizara kwa kushirikiana na wadau imefanya juhudi mbalimbali ikiwemo kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ambao utekelezaji wake utaanza Mwezi Julai, 2017 hadi Juni, 2022.
Amesema kuwa mafunzo haya yameandaliwa ili kuhakikisha kuwa Mpango Kazi huu unaeleweka na kutekelezwa ipaswavyo na wadau na Wizara imekuwa ikitoa mafunzo kuhusu Mpango huu kwa wadau mbalimbali na  mafunzo haya ya siku mbili yameandaliwa  kwa ajili ya Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa ambayo haikupata nafasi ya kushiriki katika mafunzo yaliyofanyika Mwezi Machi, 2017