Friday, 2 June 2017

Baadhi ya  Wajumbe walioshiriki mafunzo ya Mkakati wa Kitaifa Kukomesha ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto leo mjini Morogoro wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo leo jijini Morogoro.
Wajumbe walioshiriki mafunzo ya Mkakati wa Kitaifa Kukomesha ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto leo mjini Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi kutoka Wizara ya Aya(Idara kuu Maendeleo ya Jamii aliyesimamana Bwana .Charlse Mafwimbo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera akisoma hotub  kwa wajumbe wa Mkutano wa walioshiriki mafunzo ya Mkakati wa Kitaifa Kukomesha ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto leo mjini Morogoro.        
Baadhi ya  Wajumbe walioshiriki mafunzo ya Mkakati wa Kitaifa Kukomesha ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto leo mjini Morogoro wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo leo jijini Morogoro
Wanawake na watoto nchini Tanzania wamekuwa wakifanyiwa  ukatili kwa kisingizio cha mila na desturi huku jamii ikishuhudia au kusikia wanawake na watoto wakipigwa na wakati mwingine kubakwa na hata kuuwawa na watu wa karibu ikiwemo waume au wapenzi wao.
Utafiti wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2016 unaweka bayana kuwa  Nchi za Afrika zilizochini ya Jangwa la Sahara zinaingia hasara ya dolla billion 95 sawa na shilingi trilioni 212 kila mwaka kutokana na kukosa usawa wa kijinsia na  kuendelea kuwepo kwa  vitendo vya ukatili wa kijinsia. Hali  hii ni ushahidi tosha kuwa vitendo vya ukatili vina madhara makubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.
Amesema hayo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo  ya   Jinsia  Bw.Julius Mbilinyi wakati akisoma  hotuba kwa niaba ya  Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  - Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga wakati wa ufunguzi wa Mafunzo Kuhusu Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto, kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii  wa Asasi za Kiraia leo Mjini Morogoro.
Bw. Mbilinyi ameongeza kuwa tafiti  mbalimbali ikiwemo Taarifa kuhusu Idadi ya Watu na Afya wa mwaka 2015-2016  inaonesha kuwa idadi  ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa nchini bado ipo juu ambapoTaarifa hii inaonesha kuwa “wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.
Aidha Ukatili wa kimwili unaongezeka kadri umri unavyoongezeka na Asilimia 22 ya wanawake wenye umri wa miaka 15-19 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili, ukilinganisha na asilimia 48 ya wanawake wenye umri wa miaka 40-49”. 
Aliongeza kuwa madhara ya vitendo vya ubaguzi,  unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto vimeathiri na vinaendelea kuwaathiri kiafya, kisaikolojia na kijamii wahanga wa vitendo hivi. Hali hiyo pia inaathiri ushiriki wao katika shughuli za kijamii, kiuchumi, kisiasa na maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.  
Aidha katika kukabiliana na changamoto ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Wizara kwa kushirikiana na wadau imefanya juhudi mbalimbali ikiwemo kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ambao utekelezaji wake utaanza Mwezi Julai, 2017 hadi Juni, 2022.
Amesema kuwa mafunzo haya yameandaliwa ili kuhakikisha kuwa Mpango Kazi huu unaeleweka na kutekelezwa ipaswavyo na wadau na Wizara imekuwa ikitoa mafunzo kuhusu Mpango huu kwa wadau mbalimbali na  mafunzo haya ya siku mbili yameandaliwa  kwa ajili ya Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa ambayo haikupata nafasi ya kushiriki katika mafunzo yaliyofanyika Mwezi Machi, 2017

      

0 comments:

Post a Comment